Monday, September 17, 2012

FASHION



MY BEDROOM

Romantic Bedroom

Princess Bedroom

Havilland Bedroom

TODAY'S FOOD






UGALI, NYAMA, MBOGA MBOGA NA KACHUMBARI

NANI ANATAKIWA KULA : Rika Lolote.
MUDA : Mchana na Usiku.
KINYWAJI: Maji, Juice Ya Matunda, Soda.
KIFAA : Hakuna Haja ya Kifaa...Mkono unafaa.

SIMULIZI YA UKWELI

 

"Face Book Imenidharirisha !!"- (03)

 BIOGRAPHY:
Name:- SHAMSA K. ABOUD       
Umri :- 26
Kabila :- Mrangi
Anuani :- shamsa.abiud88@rocketmail.com

*************************************************************************************************

Shamsa ni Msichana ambaye anakila sifa ya kuitwa Mrembo. Nilikutana naye katika hali mabayo ninaamini hata wewe ukifuatilia kwa Ukaribu simulizi yake utachukia kile ambacho kimemkuta. Sehemu ya kwanza inaenda kama ambavyo anasimulia....KARIBU !!
*********************************************************************************************** 
 

Siku iliyofuata nilienda Chuo kama kawaida. Hammy alinitafuta kwa hali na Mali katika Simu yangu, lakini hata sikuwa na Muda wa Kumsikiliza. Nilipofika Chuo, nilimpa Mchapo wote Besti yangu Sasha. 

Hata yeye hakuamini, ilibidi tutoroke vipindi na kuelekea Internet cafee ili kumuona huyo mtu (Naseeb). Sasha hakuamini pia alichokiona. Alinipongeza sana katika hilo….huku akinisihi kuwa makini na Wavulana wa Facebook. Alijitahidi sana kunisihi kutomsaliti Hammy kwa ajili ya Naseeb, lakini sikumuelewa, maana nilihisi tayari ninampenda Naseeb. Nilimuambia nitajitahidi kuepuka Suala la mahusiano ya kimapenzi na Naseeb, kumbe tayari nilikuwa ninayangu moyoni.

Kuanzia muda huo wote, Hammy alijuta kuniamini. Ugomvi ulikuwa hauishi. Biashara yake ikaanza kwenda Kombo kutokana na muda mwingi kuutumia akinifuata chuo, akitafuta chanzo cha Mimi kubadilika. Hammy akawa haingii tena katika Biashara yake. Kaka yangu na Sasha wakawa ni wasuluhishi wa Ugomvi wetu, lakini hakuna kilichobadilika.

Baada ya Wiki kadhaa za Urafiki wangu na Naseeb, finaly akaniaproach, na mimi bila Kinyongo nikamkubalia. Hammy alikuja akagundua Hali hiyo, na kusababisha Mimi kubreak up naye maana alikuwa akinisihi kutokufanya mabaya hayo, hali niliyoiona kama ni Usumbufu kwangu na Naseeb.

Katika Muda wote huo, Sikuwahi kukutana na Naseeb uso kwa Uso. Sasha alinisihi kumrudia Hammy na Kuachana na Naseeb coz ni mtu ambaye tumeekutana naye Facebook tu, lakini mimi haikuwa sababu ya msingi Kwangu, kwani nilishakufa Nikaoza.

ITAENDELEA......................

TODAY'S COUPLE TALK.

KWANI UKWELI NI DHAMBI?.




Hakuna Kitu Kirahisi sana hapa Duniani kama Kumpenda Mpenzi Wako. Na Amini Usiamni, hakuna Kitu Kigumu sana Hapa duniani kama Kumpoteza Mpenzi wako amabaye pengine Ulitarajia kufaya Naye Mambo Mengi.

"Mamumivu ya Hisia" ni zaidi ya kuchomwa na Msumari pindi ugongeleapo Mlango katika Nyumba yako. "Chozi" la Kuachwa ama Kutendwa ama kuumizwa, ni thamani kubwa sana ambayo kamwe hainunuliki kwa gharama yoyote ile Duniani zaidi ya HISIA zitokanazo na Mapenzi na Mahaba ya Dhati.

"Kwikwi za Kilio" cha Upweke na Maumivu ya Kusalitiwa mara mia ya maumivu ya kuungua na Moto unaowaka kwa motisha na Presha ya Upepo Mkali unaovuma na kuuchochea ili uwake zaidi.

"Ukweli" wa Hisia Zako dhidi ya Yule akupendaye kwa dhati, ni zaidi ya Furaha ambayo anayo Mzazi aliyejifungua Mtoto baada ya kutaabika kwa Miezi Tisa.

Kuchezea Hisia za Mwenzako ni Mchezo ambao ushindi wake utakuja kukughalimu zaidi ya ulichonacho Maishani Mwako.
Kuwa Muwazi kwa Mpenzi Wako ili kumhakikishia Furaha ya Maisha katika Ulimwengu wa Mahaba, maana "Ukweli Sio Dhambi, bali Dhambi ni Kuuficha Ukweli kwa Mwnzi Wako."

Wednesday, August 22, 2012

SIMULIZI YA KWELI YA SHAMSA-SEHEMU YA PILI




 

FACEBOOK IMENIDHARIRISHA -Shamsa (02)

Baada ya kuchat muda Mrefu sana, nilijikuta mimi mwenyewe nikitoa namba yangu kwa Naseeb ili tuweze kuwasiliana even kwenye Simu. Nilipomaliza shughuli hiyo, nilianza safari ya kurudi Nyumbani. Nilipokuwa njiani, Hammy alinipigia simu lakini sikupokea (BOFYA "LOVE STORY")

Je Kumpiga Mwenzi wako Ni suluhu ya matatizo yenu?



Na Frank Joachim

Katika Asilimia 100 ya Jinsia ambayo huwa wanapigwa sana katika Ndoa, Uchumba, Mapenzi ya Kawaida (Girlfriends and Boyfriends), Wanawake huwa wanachukua zaidi ya Asilimia 90. Kiafrika, hii huwa inatokana na Asilia tuliyokua nayo, yaani mfumo Dume.
Ni sawa, hata Ughaibuni mambo haya hutokea, japo ni kwa asilimia ndogo, kutokana na Sheria nza Nchi Hizo, Mfano Marekani, ukimpiga Mwanamke, basi unafunguliwa mashitaka ya “Domestic Violence” na Kuwajibishwa vilivyo. Hii inakuwa inawafanya watu wengi kuepukana na mtukio hayo ya uonevu wa Kijinsia.

Kwa Nini Tunapiga (Wanaume)



Kulinda Hadhi na Heshima.
Hakuna Jinsia ambayo huwa inathamini hadhi yake binafsi kama Jinsia Ya Kiume. Hii inatokana na mfumo dume uliorithishwa na Wazazi wetu wa Awali, yaani Mababu zetu, ambapo huwa mwanaume anahisi kuwa yeye ni bora na anastahili kuboreshewa ubora wake ili kutambulika katika Jamii inayomzunguka.
Endapo Mwanamke ataonesha dharau, Kiburi, kutokutekeleza baadhi ya Majukumu aliyokabidhiwa na Mwanamume (Mpenzi, mchumba, au Mume), basi ataadhibiwa kwa Kipigo chochote kile ili kuilinda Hadhi yake na Heshima yake isije ikashuka.

Hasira za Karibu

Hii ni sawa kabisa, hasa kwa Wanaume. Kuna baadhi ya Wanaume ambao kiujumla huwa ni Wepesi wa kuchukia haraka, na kuchukua hatua kadhaa mkononi. Kuna baadhi ya Wanaume ambao huwa hawafanyi hivyo. Mwanaume wa aina hii (Kuchukia Mapema) mara nyingi huwaadhibu sana Wapenzi wao. Nimewahi kuishi na rafiki yangu wa aina hii. Ilikuwa ikipita wiki Nzima mpenzi wake hajalia, basi jamaa atakuwa hayupo, au anaumwa. Jambo hili lilikuwa likimnyima raha sana Mpenzi wake, kitu ambacho kingepa athari kubwa ya Kisaikolojia Msichana Yule, endapo wasingetengana

Ulimbukeni/ Kuiga/ Sifa za Kijinga.

Kuna mwanaume mwingine anaweza akawa anahisi ni sifa mbele ya wenzake kusema kuwa amempiga mpenzi wake. Hii ni kutaka kujionesha kuwa ana mamlaka makubwa sana na ni sifa madhubuti kumpiga Mwenzi wake. Mwingine anaweza akawa anamuona Frank anapiga sana Mpenzi wake, na bado wanaendelea kuwa pamoja, basi na yeye anaamua kumpiga Ngum,I, makofi n.k ilimradi tu awe kama Frank, jambo ambalo sio unjanja wala nini !!

 Kwa nini anapenda Kupigwa? (Wanawake)

Kudhirisha kama anapendwa.

Zamani nilikuwa Siamini kama mwanamke anapenda kupigwa. Nilikuwa ninadhani kuwa wanawasikinzia. Katika Mapenzi ya sasa Hivi, yaani Rika letu sisi vijana, Nilibaini kuwa, kuna wanawake au mabinti wanapenda na huwa wanalazimisha kupigwa kwa kufanya makosa maksudi. Hii ni kutaka kubaini kama mpenzi wake anampenda au Laa.

Kuiga/ Ulimbukeni

Amini Usiamini, kuna wanawake ambao wakisika wenzao wakisimulia kuwa wamepigwa basi wanafurahi na kutramani na wao kupigwa. Basi watafanya kila wafanyalo au wawezalo ili kuhakikisha kuwa wanapigwa na wapenzi wao ili kujua radha yake ikoje.

ATHARI;

Athari huwa ni kubwa sana katika Hilo.
Kujeruhi
Kuua,
Kuathiri/ Kuathirika Kisaikolojia., n.k