PROMO BRAND 1
WACKAVVU FASHION
Monday, September 17, 2012
TODAY'S FOOD
UGALI, NYAMA, MBOGA MBOGA NA KACHUMBARI
NANI ANATAKIWA KULA : Rika Lolote.
MUDA : Mchana na Usiku.
KINYWAJI: Maji, Juice Ya Matunda, Soda.
KIFAA : Hakuna Haja ya Kifaa...Mkono unafaa.
SIMULIZI YA UKWELI
"Face Book Imenidharirisha !!"- (03)
BIOGRAPHY:
Name:- SHAMSA K. ABOUD
Umri :- 26
Kabila :- Mrangi
Anuani :- shamsa.abiud88@rocketmail.com
*************************************************************************************************
Shamsa
ni Msichana ambaye anakila sifa ya kuitwa Mrembo. Nilikutana naye
katika hali mabayo ninaamini hata wewe ukifuatilia kwa Ukaribu simulizi
yake utachukia kile ambacho kimemkuta. Sehemu ya kwanza inaenda kama
ambavyo anasimulia....KARIBU !!
***********************************************************************************************
Siku iliyofuata nilienda Chuo kama kawaida. Hammy
alinitafuta kwa hali na Mali katika Simu yangu, lakini hata sikuwa na Muda wa
Kumsikiliza. Nilipofika Chuo, nilimpa Mchapo wote Besti yangu Sasha.
Hata yeye
hakuamini, ilibidi tutoroke vipindi na kuelekea Internet cafee ili kumuona huyo
mtu (Naseeb). Sasha hakuamini pia alichokiona. Alinipongeza sana katika
hilo….huku akinisihi kuwa makini na Wavulana wa Facebook. Alijitahidi sana
kunisihi kutomsaliti Hammy kwa ajili ya Naseeb, lakini sikumuelewa, maana
nilihisi tayari ninampenda Naseeb. Nilimuambia nitajitahidi kuepuka Suala la
mahusiano ya kimapenzi na Naseeb, kumbe tayari nilikuwa ninayangu moyoni.
Kuanzia muda huo wote, Hammy alijuta kuniamini. Ugomvi
ulikuwa hauishi. Biashara yake ikaanza kwenda Kombo kutokana na muda mwingi
kuutumia akinifuata chuo, akitafuta chanzo cha Mimi kubadilika. Hammy akawa
haingii tena katika Biashara yake. Kaka yangu na Sasha wakawa ni wasuluhishi wa
Ugomvi wetu, lakini hakuna kilichobadilika.
Baada ya Wiki kadhaa za Urafiki wangu na Naseeb, finaly
akaniaproach, na mimi bila Kinyongo nikamkubalia. Hammy alikuja akagundua Hali
hiyo, na kusababisha Mimi kubreak up naye maana alikuwa akinisihi kutokufanya
mabaya hayo, hali niliyoiona kama ni Usumbufu kwangu na Naseeb.
Katika Muda wote huo, Sikuwahi kukutana na Naseeb uso kwa
Uso. Sasha alinisihi kumrudia Hammy na Kuachana na Naseeb coz ni mtu ambaye
tumeekutana naye Facebook tu, lakini mimi haikuwa sababu ya msingi Kwangu,
kwani nilishakufa Nikaoza.
ITAENDELEA......................
TODAY'S COUPLE TALK.
KWANI UKWELI NI DHAMBI?.
Hakuna Kitu Kirahisi sana hapa Duniani kama Kumpenda Mpenzi Wako. Na Amini Usiamni, hakuna Kitu Kigumu sana Hapa duniani kama Kumpoteza Mpenzi wako amabaye pengine Ulitarajia kufaya Naye Mambo Mengi.
"Mamumivu ya Hisia" ni zaidi ya kuchomwa na Msumari pindi ugongeleapo Mlango katika Nyumba yako. "Chozi" la Kuachwa ama Kutendwa ama kuumizwa, ni thamani kubwa sana ambayo kamwe hainunuliki kwa gharama yoyote ile Duniani zaidi ya HISIA zitokanazo na Mapenzi na Mahaba ya Dhati.
"Kwikwi za Kilio" cha Upweke na Maumivu ya Kusalitiwa mara mia ya maumivu ya kuungua na Moto unaowaka kwa motisha na Presha ya Upepo Mkali unaovuma na kuuchochea ili uwake zaidi.
"Ukweli" wa Hisia Zako dhidi ya Yule akupendaye kwa dhati, ni zaidi ya Furaha ambayo anayo Mzazi aliyejifungua Mtoto baada ya kutaabika kwa Miezi Tisa.
Kuchezea Hisia za Mwenzako ni Mchezo ambao ushindi wake utakuja kukughalimu zaidi ya ulichonacho Maishani Mwako.
Kuwa Muwazi kwa Mpenzi Wako ili kumhakikishia Furaha ya Maisha katika Ulimwengu wa Mahaba, maana "Ukweli Sio Dhambi, bali Dhambi ni Kuuficha Ukweli kwa Mwnzi Wako."
Subscribe to:
Posts (Atom)














