Monday, September 17, 2012

SIMULIZI YA UKWELI

 

"Face Book Imenidharirisha !!"- (03)

 BIOGRAPHY:
Name:- SHAMSA K. ABOUD       
Umri :- 26
Kabila :- Mrangi
Anuani :- shamsa.abiud88@rocketmail.com

*************************************************************************************************

Shamsa ni Msichana ambaye anakila sifa ya kuitwa Mrembo. Nilikutana naye katika hali mabayo ninaamini hata wewe ukifuatilia kwa Ukaribu simulizi yake utachukia kile ambacho kimemkuta. Sehemu ya kwanza inaenda kama ambavyo anasimulia....KARIBU !!
*********************************************************************************************** 
 

Siku iliyofuata nilienda Chuo kama kawaida. Hammy alinitafuta kwa hali na Mali katika Simu yangu, lakini hata sikuwa na Muda wa Kumsikiliza. Nilipofika Chuo, nilimpa Mchapo wote Besti yangu Sasha. 

Hata yeye hakuamini, ilibidi tutoroke vipindi na kuelekea Internet cafee ili kumuona huyo mtu (Naseeb). Sasha hakuamini pia alichokiona. Alinipongeza sana katika hilo….huku akinisihi kuwa makini na Wavulana wa Facebook. Alijitahidi sana kunisihi kutomsaliti Hammy kwa ajili ya Naseeb, lakini sikumuelewa, maana nilihisi tayari ninampenda Naseeb. Nilimuambia nitajitahidi kuepuka Suala la mahusiano ya kimapenzi na Naseeb, kumbe tayari nilikuwa ninayangu moyoni.

Kuanzia muda huo wote, Hammy alijuta kuniamini. Ugomvi ulikuwa hauishi. Biashara yake ikaanza kwenda Kombo kutokana na muda mwingi kuutumia akinifuata chuo, akitafuta chanzo cha Mimi kubadilika. Hammy akawa haingii tena katika Biashara yake. Kaka yangu na Sasha wakawa ni wasuluhishi wa Ugomvi wetu, lakini hakuna kilichobadilika.

Baada ya Wiki kadhaa za Urafiki wangu na Naseeb, finaly akaniaproach, na mimi bila Kinyongo nikamkubalia. Hammy alikuja akagundua Hali hiyo, na kusababisha Mimi kubreak up naye maana alikuwa akinisihi kutokufanya mabaya hayo, hali niliyoiona kama ni Usumbufu kwangu na Naseeb.

Katika Muda wote huo, Sikuwahi kukutana na Naseeb uso kwa Uso. Sasha alinisihi kumrudia Hammy na Kuachana na Naseeb coz ni mtu ambaye tumeekutana naye Facebook tu, lakini mimi haikuwa sababu ya msingi Kwangu, kwani nilishakufa Nikaoza.

ITAENDELEA......................

No comments:

Post a Comment