KWANI UKWELI NI DHAMBI?.
Hakuna Kitu Kirahisi sana hapa Duniani kama Kumpenda Mpenzi Wako. Na Amini Usiamni, hakuna Kitu Kigumu sana Hapa duniani kama Kumpoteza Mpenzi wako amabaye pengine Ulitarajia kufaya Naye Mambo Mengi.
"Mamumivu ya Hisia" ni zaidi ya kuchomwa na Msumari pindi ugongeleapo Mlango katika Nyumba yako. "Chozi" la Kuachwa ama Kutendwa ama kuumizwa, ni thamani kubwa sana ambayo kamwe hainunuliki kwa gharama yoyote ile Duniani zaidi ya HISIA zitokanazo na Mapenzi na Mahaba ya Dhati.
"Kwikwi za Kilio" cha Upweke na Maumivu ya Kusalitiwa mara mia ya maumivu ya kuungua na Moto unaowaka kwa motisha na Presha ya Upepo Mkali unaovuma na kuuchochea ili uwake zaidi.
"Ukweli" wa Hisia Zako dhidi ya Yule akupendaye kwa dhati, ni zaidi ya Furaha ambayo anayo Mzazi aliyejifungua Mtoto baada ya kutaabika kwa Miezi Tisa.
Kuchezea Hisia za Mwenzako ni Mchezo ambao ushindi wake utakuja kukughalimu zaidi ya ulichonacho Maishani Mwako.
Kuwa Muwazi kwa Mpenzi Wako ili kumhakikishia Furaha ya Maisha katika Ulimwengu wa Mahaba, maana "Ukweli Sio Dhambi, bali Dhambi ni Kuuficha Ukweli kwa Mwnzi Wako."


No comments:
Post a Comment