"Face Book Imenidharirisha !!"- (01)
BIOGRAPHY:Name:- SHAMSA K. ABOUD
Umri :- 26
Kabila :- Mrangi
Anuani :- shamsa.abiud88@rocketmail.com
*************************************************************************************************
Shamsa ni Msichana ambaye anakila sifa ya kuitwa Mrembo. Nilikutana naye katika hali mabayo ninaamini hata wewe ukifuatilia kwa Ukaribu simulizi yake utachukia kile ambacho kimemkuta. Sehemu ya kwanza inaenda kama ambavyo anasimulia....KARIBU !!
***********************************************************************************************
“Sikuwa mfahamu sana katika suala zima la Facebook, licha ya
kwamba nilikuwa nikiwaona Rafiki zangu wengi sana wakiitumia, huku baadhi yao
Wakiisifia. Obviously, nilipata hamu kubwa sana ya kutaka kufahamu kilichokuwa
kikiendelea ndani ya Mtandao huo. If am not mistaken, it was 2010 ndo nilianza
kusikia habari hizo za Facebook. By that time nilikuwa nachukua Diploma in AIR
TICKETING katika chuo kimoja hivi hapa Jijini Dar es Salaam.
Nilijitahidi sana kuweza kuficha hali halisi y kuwa na hamu
ya kujiunga na Facebook, lakini nilishindwa. Nilichukua uamuzi wa kumwambia
rafiki yangu ambaye alikuwa ni Jirani yangu Darasani. She was known as Sasha
(Salma SHareef). Nilipomuambia duku duku langu, hakukataa, na aliniahidi kuwa
tutakapomaliza tu Vipindin hapo College, tutapitia Internet Cafee ili anisaidie
kujinga coz hata yeye tayari alikuwa ni among of members. Kweli, Sasha akafanya
kama alivyoniahidi, tukafungua account, nikaweka Picha ya Rihana kama ya kuanza
nayo coz nilikuwa sina picha by that moment. Namshukuru Sasha coz She taught me
how to use it na nikajitahidi sana kujifunza.
Suddenly kama Wiki mbili hivi, nilijikuta Napata marafiki
wengi sana hasa wale ambao nilisoma nao O level, A level, Chuo, na wengine
ambao waliona picha zangu baada ya kuziweka kwenye Account yangu.
By that time nilikuwa na Boyfriend ambaye alinipenda sana na
mimi kufanya hivyo. He was called Hamidu but mi nilipenda sana kumuita “Hammy”.
Alikuwa ni mfanya biashara wa Nguo za Mitumba katika Soko la Big Brother pale
Urafiki. Offcourse tulipendana sana, na kila nilichohitaji alikuwa tayari
kukitoa japo kwa Uchache. Hatukuwahi kupigana, hatukuwahi kuwa na Conflict
kubwa kubwa, but zilikuwa ni za kawaida sana kwa wapenzi. My Hammy alikuwa
hajui kutumia Computer, so hakuwa facebook member. Frankly speaking alinipenda
sana na nilimpenda sana
Baada ya Mwezi kama Mmoja hivi, nilikuwa tayari mtaalamu wa
facebook. Nilijiunga na Groups Kibao, Nilikuwa kila nikiamka, nnawaza picha
mpya ya Kuweka facebook, post Mpya, na kuingia inbox kusoma SMS za rafiki
zangu. So facebook ikawa facebook Chuo, Nyumbani, Mitaani na hata kuanza ugomvi
na Hammy, coz alipokuwa akihitaji kuongea na mimi au kukutana, ninamjibu
“Hammy, Niko Facebook nw, ntakucheki Badae”. But the cute guy alinivumilia
hivyo hivyo though kila siku ilikuwa Lazima Tugombane.
Siku moja nikiwa Internet Cafee ya Mtaa wa Home, nilikutana
Na Friend Request Moja tu na haikuwa kawaida yangu. Nilipoifunguingua tu,
nilikutana na Jina “NASEEB-The Don Killer”, jina lililonishawishi kuingia
katika Profile yake. Huwezi amini sikuamini nilichokiona. He was so Handsome
asikuambie Mtu. Nikajaribu kuingi katika picha zake ndo kabisaaaa….nilipagawa.
Suddeenly, nikajikuta ninaaccept request yake na kuanza kucoment kwenye Picha
zake na Post zake. Wakati nikifanya zoezi hilo, ghafla akanitumia message
kwenye Chat space yangu, ikimaanisha by that time alikuwa online pia. Sikuwa na
tatizo, nikaanza kumjibu. Chati ikawa kuchat, Muda ukawa unaongezwa bila Tatizo
coz money ilikuwepo.
Nilinogewa sana na Chating yangu na NASEEB “The Don Killer”.
He was so sweet in writing,convincing to reply his texts, na vitu vingine
vingi. Zilipigwa simu nyingi sana by then, lakini sikuweza kupokea coz of
Naseeb. Hammy was among of watu walionipigia sana
##################################################################
Name:- SHAMSA K. ABOUD
Umri :- 26
Kabila :- Mrangi
Anuani :- shamsa.abiud88@rocketmail.com
*************************************************************************************************
#####################################################################
##################################################################
"Face Book Imenidharirisha !!"- (02)
BIOGRAPHY:Name:- SHAMSA K. ABOUD
Umri :- 26
Kabila :- Mrangi
Anuani :- shamsa.abiud88@rocketmail.com
*************************************************************************************************
Shamsa
ni Msichana ambaye anakila sifa ya kuitwa Mrembo. Nilikutana naye
katika hali mabayo ninaamini hata wewe ukifuatilia kwa Ukaribu simulizi
yake utachukia kile ambacho kimemkuta. Sehemu ya kwanza inaenda kama
ambavyo anasimulia....KARIBU !!
***********************************************************************************************
Baada ya kuchat muda Mrefu sana, nilijikuta mimi mwenyewe
nikitoa namba yangu kwa Naseeb ili tuweze kuwasiliana even kwenye Simu.
Nilipomaliza shughuli hiyo, nilianza safari ya kurudi Nyumbani. Nilipokuwa
njiani, Hammy alinipigia simu lakini sikupokea. Alipiga sana lakini bado
nilizipuuzia. Kumbe alikuwa nyuma yangu. Nilishtuka sana aliponiita, huku
akianza kunilaumu kwanini sipokei simu zake. I remember nilimjibu kuwa sikuwa
kwenye Mood Nzuri ya kuongea naye. He didn’t believe that Lie hali ilyomfanya
kuanza kunifokea. Wakati akinfanya hayo, ghafla iliingia simu huku ikiwa na
namba ngeni. Direct niliamini kuwa huyo atakuwa ni Naseeb. Haraka nilipokea ile
Simu huku nikimuogopa Hammy. Kweli alikuwa ni yeye. My god, Kijana alikuwa ana
sweet Sound when talking through the Phone. Ilinibidi nimwambie kuwa
nitamtafuta Baadaye maana sikuwa Sehemu nzuri, hali iliyomfanya Hammy achukie
zaidi na Kunipiga kofi mara baada ya kukata Simu. Haukuwa ugomvi mdogo kwetu,
hali iliyonifanya nianze kumdhalilisha Hammy wangu infront of The mass.
Kutokana na hali hiyo, sikutaka kuongea wala kukutana tena
na Hammy, japo alinifuata huku akinisihi nimpe msamaha wangu. Nilipofika home,
nilisimulia kaka angu coz alikuwa ni Rafiki yngu wa Karibu Sana. Alinisihi
nisimchukie hivyo Hammy mana nimetoka naye mbali, na ni mwanaume pekee ambaye
hunifanya niwe happy Siku zote. Nilijitahidi kumsikiliza kaka, lakini haikuwa
vile. Nilikuwa nasubiri muda wa kulala ukifika nimshtue Naseeb “The Don
Killer”.
Kama ambvyo nilikuwa nimemuahidi Naseeb, nilimpigia baada ya
kuingia Chumbani kwangu kwa ajili ya Kulala. Tulizunumza mengi sana ukizingatia
nilikuwa nimejipanga haswa. Naseeb aliniambia yeye ni Mfanya biashara wa Magari
kutoka Nje, yaani huwa anaagiza kwa njia ya Mtandao na kuwapelekea wale watu
waliompatia Hitaji la gari. Hakuwa na Show room, alikuwa anafanya kwa Order.
Basi, baada ya kuzungumza na Naseeb majira ya saa nane
Usiku, nilikuta Missed Calls nyingi za Hammy, lakini sikusumbuka Kumtafuta,
badala yake nilizima Simu na kuuchapa
usingizi hadi asubuhi.
#####################################################################



No comments:
Post a Comment